Tangazo: Tovuti ya salayapapa.org inapatikana hewani.

TANGAZO: MTANDAO WA SALA WA PAPA SASA UNAPATIKANA KUPITIA TOVUTI YETU YA KISWAHILI

Tunayo furaha kubwa kutangaza kwamba Mtandao wa Sala wa Papa sasa unapatikana kupitia tovuti yetu mpya ya Kiswahili: salayapapa.org. Tovuti hii inashughulikia mada zote zinazohusu Mtandao wa Sala wa Papa duniani na inapatikana kwa lugha mbili, Kiswahili na Kiingereza, kwa ajili ya hadhira yetu ya Afrika Mashariki.

Manufaa ya kufuatilia muduma zetu mtandaoni:

  • Upatikanaji wa Haraka: Tovuti yetu inawawezesha wakristo kupata taarifa za hivi punde kuhusu nia za maombi za Papa na huduma nyingine muhimu.
  • Ushiriki katika sala: Kupitia tovuti, unaweza kushiriki katika ibada na sala zinazotolewa na Mtandao wa Sala wa Papa kupitia simu yako.
  • Elimu na Mafunzo: Tunatoa vipeperushi na miongozo kuhusu “Njia ya Moyo” na Nguzo nyingine za Utume wa Sala, ili kusaidia waumini kuelewa na kushiriki kikamilifu.

Tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii, ambako tunakaribisha maoni na mrejesho kuhusu jinsi tunavyoweza kuboresha huduma zetu zaidi.

Jiunge Nasi Leo:

Tembelea tovuti yetu salayapapa.org kwa taarifa zaidi na kufaidika na huduma mbalimbali za Mtandao wa Sala wa Papa. Tuendelee kushirikiana katika kueneza upendo na huruma ya Mungu kupitia sala na matendo ya huruma.

Karibuni nyote na Mungu awabariki!

Leave a Reply