Karibu!
Mtandao wa Sala wa Baba Mtakatifu (Utume wa Sala) ni huduma ya kikanisa iliyo idhinishwa na Baba Mtakatifu chini ya uangalizi wa Shirika la Yesu. Tunajihusisha na changamoto ulimwenguni na zinazokabili utume wa Kanisa. Changamoto hizi huainishwa kupitia nia za sala za kila mwezi za Baba Mtakatifu. Mtandao wa Sala wa Baba Mtakatifu unawaalika wote kusali na kuchukua hatua juu ya changamoto zilizopo ulimwenguni, zile zinazokabili utume wa Kanisa, na zinazotambulika na Baba Mtakatifu katika nia zake za kila mwezi. Nia hizi za sala ni muhimu sana kwa maisha yetu ya sala na utume wetu.
Historia ya Utume wa Sala
Utume wa Sala ulianzishwa mwaka 1844 huko Ufaransa. Mwaka 1866, katiba yake ya kwanza ilikubaliwa na Papa Pius IX, na mwaka 1896 ilifanyiwa marekebisho na Papa Leo XIII. Mwaka 1951, Papa Pius XII alikubali katiba hiyo mpya. Mwaka 2018, Baba Mtakatifu aliweka Mtandao wa Sala wa Papa kuwa Kazi ya Kipapa ili kusisitiza asili ya utume huu ulimwenguni kote na umuhimu wa kusali zaidi na kwa dhati kutoka moyoni. Mtandao wa sala wa papa una taratibu mbalimbali za malezi ili kutuvuta karibu na moyo wa Yesu na kutuunganisha kwa karibu na nia na mapenzi yake. Sala ya papa inatualika tujiunge na utume ambao Yesu alipokea kutoka kwa Baba. Kama marafiki wa Yesu, tunatambua changamoto za dunia na kujitolea kwa sala na huduma kila mwezi.